Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif amesema nchi yake itajibu vikali baada ya pande hizo mbili kushambuliana usiku kucha katika eneo la mpakani. Waziri Mkuu, wa Pakistan amelaumu mamlaka ya Taliban kwa kuruhusu ardhi yao kutumiwa na magaidi.

Je Afghastan inasemaje

Kwa upande wa Afghanistan, msemaji mkuu wa serikali ya Taliban, Zabihullah Mujahid, amesema vikosi vya Afghanistan vimekamata vituo 25 vya jeshi la Pakistan, wanajeshi 58 wa Pakistan wameuliwa na wengine 30 wamejeruhiwa katika oparesheni hiyo na kwamba hayo yalikuwa majibu ya ukiukaji wa mara kwa mara kwenye anga na ardhi yake unaofanywa na Pakistan.

Mapema wiki hii mamlaka ya Afghanistan iliilaumu Pakistan kwa kuushambulia kwa mabomu mji mkuu, Kabul, na soko mashariki mwa nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *