
Marekani imetangaza hatua hiyo baada ya China kutangaza sera ya kudhibiti madini yake ya udongo adimu. Kwa upande wake China imetishia kuchukua hatua zinazolingana na za Marekani ili kulinda haki na maslahi yake.
Msemaji wa wizara ya biashara ya China ameeleza kuwa tamko la Marekani ni mfano dhahiri wa ugeugeu wa nchi hiyo. China imesema ikiwa Marekani itaendelea na sera hiyo nayo itachukua hatua thabiti kuyalinda maslahi yake.
Ushuru wa Trump
Hatua hiyo ya mvutano wa pande hizo mbili inatishia kuanzisha upya vita vya kibiashara vilivyoanza mwanzoni mwa mwaka huu muda mfupi baada ya Trump alipoingia madarakani. Marekani na China zilisitisha kuwekeana ushuru mkubwa baada ya duru kadhaa za mazungumzo.