
Nchi ya Ufaransa imekumbwa na msukosuko wa kisiasa tangu Rais Emmanuel Macron alipoitisha kura ya mapema mwaka jana ambapo alitarajia ingeimarisha mamlaka yake lakini badala yake kura hiyo ilisababisha matokeo yaliyouimarisha upinzani unaoegemea mrengo mkali wa kulia.
Sebastia Lecornu arejeshwa madarakani
Macron alimrejesha Lecornu, Ijumaa siku nne tu baada ya waziri mkuu huyo kujiuzulu na serikali yake ya kwanza kuanguka. Waziri huyo wa zamani wa ulinzi lazima sasa aunde serikali na kuwasilisha rasimu ya bajeti ya mwaka ujao wa 2026 kabla ya tarehe ya mwisho ambayo ni siku ya Jumanne tarehe 13 mwezi huu ili bunge liwe na siku 70 za kikatiba za kuichunguza bajeti hiyo kabla mwaka kumalizika.
Chama cha mrengo wa kulia cha Republican (LR) mshirika mkuu wa kisiasa, kiliwapa pigo kubwa wanachama wa chama cha Rais Macron cha Renaissance (RE) pale kilipotangaza kuwa hakitashiriki katika serikali mpya na badala yake kinataka kitashirikiana na serikali mpya katika kupitisha miswaada watakayoridhia.