
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametoa taarifa leo inayosema kwamba watu wapatao 42 wamefariki kwenye ajali ya basi iliyotokea katika eneo la milimani Kaskazini mwa nchi hiyo.
Abiria 49 wamejeruhiwa. Ajali hiyo ilitokea Jumapili mwendo wa saa kumi na mbili jioni kwenye barabara kuu ya N1 karibu na mji wa Louis Trichardt, karibu kilomita 400 kaskazini mwa mji mkuu, Pretoria.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo wengi waliofariki katika ajali hiyo kwenye mkoa wa Limpopo, ni raia kutoka Zimbabwe na Malawi waliokuwa wakielekea katika mataifa yao kutoka mji wa Gqeberha huko Cape Mashariki.
Ramaphosa amesikitishwa na ajali hiyo akisema ni huzuni kwa waafrika Kusini, Zimbabwe na Malawi kwa ujumla.