
Rais Emmanuel Macron amesema ataendelea kuiongoza Ufaransa kuhakikisha uthabiti wa taifa hilo na kupuuza miito inayotolewa na kambi ya upinzani ya kumtaka ajiuzulu.
Upinzani umeongeza shinikizo dhidi ya uongozi wa Macron baada ya siku chache zilizopita kumteua tena waziri mkuu aliyejiuzulu, Sebastien Lecornu kuongoza serikali.
Rais Macron amewaambia waandishi habari akiwa nchini Misri kwamba wajibu aliokabidhiwa na wananchi wa Ufaransa ni kuwatumikia na kuwapatia ufumbuzi wa maswali wanayojiuliza kila siku.
Ufaransa iko katikati ya mgogoro mbaya wa kisiasa ambao haujawahi kuonekana kwa miongo kadhaa.