
Viongozi wakuu 19 wa nchi na serikali watahudhuria baadae leo mkutano wa hafla ya kusainiwa makubaliano ya amani ya kumaliza vita Gaza, katika mji wa kitalii wa Sharm El Sheikh nchini Misri.
Rais wa Marekani Donald Trump Emmanuel Macron na Waziri mkuu Keir Starmer wa Uingereza pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na rais wa baraza la Ulaya Antonio Costa ni miongoni mwa watakaohudhuria.
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz ambaye amesema nchi yake itasimamia utekelezaji wa mpango huo wa amani unaoungwa mkono na Marekani, ameelekea Misri kushiriki hafla hiyo ambayo pia itahudhuriwa na rais wa Mamlaka ya Wapalestina Mahmoud Abbas.