
Rais wa Madagascar Andry Rajoelina ameondolewa nchini kwa ndege ya kijeshi ya Ufaransa mnamo Oktoba 12, 2025, RFI inaweza kuthibitisha hili. Makubaliano na Rais Emmanuel Macron yaliripotiwa kuruhusu kuondolewa kwa rais huyo nchini.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mamlaka za Ufaransa zinabainisha kwamba haziingilii kwa njia yoyote katika mgogoro wa Madagascar. Nchi hiyo imekumbwa na misukosuko tangu Septemba 25 kutokana na maandamano yaliyokandamizwa kupinga kukatwa kwa maji na umeme, maandamano ambayo yaligeuka kuwa maandamano dhidi ya serikali na kutaka mkuu wa nchi ajiuzulu, pamoja na mambo mengine.
Rais wa Madagascar Andry Rajoelina aliondolewa nchini siku ya Jumapili na ndege ya kijeshi ya Ufaransa. Inaaminika kuwa hayuko tena katika ardhi ya Ufaransa, na hatima yake bado haijulikani.
Makubaliano kati ya rais kwa rais yamewezesha kuondoka kwa rais Andry Rajoelina. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kulingana na vyanzo vilivyo karibu na suala hilo, ameidhinisha kuondoka kwake. Mlolongo wa matukio ni kama ifuatavyo: jana, helikopta ilimpeleka rais wa Madagascar hadi Kisiwa cha Sainte-Marie, kwenye pwani ya mashariki ya Madagascar, na kutoka huko, alipanda ndege ya kijeshi ya Ufaransa hadi Kisiwa cha Réunion, kabla ya kuondoka na familia yake hadi Mauritius au Dubai katika Falme za Kiarabu. Kulingana na vyanzo vya RFI, rais Rajoelina hayuko tena katika Kisiwa cha Réunion.
Paris inasisitiza kwa uthabiti kwamba Ufaransa haitaingilia kijeshi kwa hali yoyote ile.
Kuondoka huku kuliidhinishwa kuruhusu mabadiliko ya amani, lakini Paris inasisitiza kwa uthabiti kwamba Ufaransa haitaingilia kijeshi Madagascar kwa hali yoyote ile. Vikosi vya kijeshi vya Ufaransa vilivyo kusini mwa Bahari ya Hindi, vinavyopiga kambi katika Kisiwa cha Réunion, havitakwenda mbali zaidi; hakutakuwa na kuingilia kati katika kisiwa hicho, wanasisitiza.
“Rais wa Jamhuri, Andry Rajoelina, atahutubia raia Madagascar leo saa 1,” ofisi ya rais wa Jamhuri ya Madagascar imebainisha mapema Oktoba 13, 2025, kwenye ukurasa wake wa Facebook.