Kuishi watu wengi katika familia moja ni jambo linaloendelea kujadiliwa katika jamii nyingi, hasa kwa kuzingatia mabadiliko ya maisha ya kisasa. Wapo wanaoona ni maendeleo, wakisema mfumo huu hujenga umoja, kusaidiana kiuchumi na kutoa malezi bora kwa watoto kupitia ushirikiano wa wazazi, babu, bibi na ndugu wengine.
Hata hivyo, wengine wanaona hali hiyo kama kurudi nyuma kutokana na changamoto kama ukosefu wa faragha, migogoro ya kifamilia na mzigo mkubwa wa gharama za maisha.
Je, kuishi watu wengi katika familia moja ni maendeleo au kurudi nyuma Tuandikie maoni yako na tutayasoma katika #KilingeChaFamilia kinachoruka kila Jumapili kuanzia saa 1:00 Usiku #UTV
#AzamTVUpdates