Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema katika sekta ya uwezeshaji wa kiuchumi hawaachi mtu …Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema katika sekta ya uwezeshaji wa kiuchumi hawaachi mtu …

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema katika sekta ya uwezeshaji wa kiuchumi hawaachi mtu wakiwemo watu wenye ulemavu ili kuboresha maisha yao.
Dkt Samia ameeleza hayo leo Jumatatu Oktoba 13, 2025 akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Nyawilimilwa mkoani Geita, katika mwendelezo wa kampeni za kusaka kura mkoani hapa.

“Kama vile ambavyo tunakuwa hatuaachi katika afya, elimu jumuishi ambayo ndugu zangu wenye ulemavu wamo, tumewashughulikia kikamilifu pamoja na vifaa vyao,”
“Vile kwenye uwezeshaji, ukiangalia katika kitabu kidogo (kitabu cha ilani cha CCM cha mkoa), kuhusu uwezeshaji kinasema baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kwa mwaka 2020/25 ni pamoja na kuongeza kwa mikopo ya asilimia 10,”

Mbali na mikopo ya asilimia 10, Dkt Samia ambaye ni Mwenyekitin wa CCM, ameeleza kuwa baadhi ya watu wenye ulemavu wanapitia kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (Tasaf).
Dkt Samia amesema kwa upande wa michezo, Serikali haijawaacha nyuma wenye ulemavu akisema kuna timu ya Taifa inayowajumuisha ambayo imekuwa ikifanya vizuri nje ya nchi.

“Niseme tu tumewazingatia (wenye ulemavu) kwenye ilani iliyopita kwa kufanya kazi nzuri, lakini pia hata katika ilani ya sasa tumewazingatia. Tupo pamoja, tumewajumuisha kwenye maendeleo nanyi ni Watanzania,
“Wanasema hatuachi mtu nyuma, yeyote kwa hali yoyote, hataachwa nyuma,” amesisitiza Dkt Samia.
#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *