Umma mkubwa wa Wapalestina, umejitokeza katika mji wa Ramallah, Ukingo wa Magharibi katika mamlaka ya Wapalestina kuwapokea wafungwa wakipalestina walioachiwa huru na Israel hivi leo Jumatatu, chini ya mpango wa makubaliano ya kusitisha vita Gaza.

Wapalestina walioachiwa huru walionekana wakiwa na furaha wakipokelewa na jamaa zao, baadhi wakinyanyua mikono kuonesha ishara ya amani huku wengine wakionekana kushindwa kutembea wenyewe bila msaada wakati wakiteremshwa kutoka kwenye basi.

Mamia ya Wapalestina wamesikika wakimshukuru mwenyezi Mungu kwa kusema Allahu Akbar baada ya kuona wenzao waliokuwa wanashikiliwa katika jela za Israel.

Miongoni mwa Wapalestina watakaoachiliwa chini ya mpango wa usitishaji vita Gaza, ni pamoja na maafisa 250 wa usalama, wakiwemo walioshtakiwa kwa mauaji ya Waisrael pamoja na kiasi 1.700 waliokamatwa na jeshi la Israel  katika Ukanda wa Gaza wakati wa vita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *