#HABARI:Katika Kuunga Mkono Juhudi za Serikali kwenye Kada ya Afya, Jeshi la Kujenga Taifa Kupitia Kampuni yake ya Ujenzi (SUMAJKT Construction Co. Ltd) limeendelea kutekeleza miradi mbalimbali nchini, ukiwemo Ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga, linalogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 6.5.
Akizungumzia mradi huo Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt. Baraka Msumi amesema SUMAJKT, limeaminika na kupewa kazi hiyo kutokana na ubora wa majengo ambayo wamekuwa wakiyajenga katika hospitali hiyo, likiwemo Jengo Kuu la wagonjwa wa nje pamoja na Jengo la Uchunguzi.
Kwa Upande wake Meneja wa Ujenzi (SUMAJKT) Kanda ya Ziwa Magharibi Meja Hamad Matata, amesema kupitia miradi hiyo ya kimkakati, Shirika linaendelea kuwa sehemu ya Huduma za Jamii.
Aidha Meneja wa Mradi huo Mkadiriaji Majenzi Arch. Mashala Mboje amesema mradi umefikia katika Hatua nzuri na hivyo upo mbioni kukamilika, ili kuwasaidia wananchi kutika huduma bora za afya.