Mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 13, 2025 amefika Chato, mkoani Geita, nyumbani kwa familia na sehemu alipozikwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na kuweka shada la maua, pamoja na kumuombea dua.

Dkt. Samia amefika kwenye makaburi hayo ya familia Rubambangwe, Chato akiambatana na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Asha- rose Migiro na baadhi ya wanafamilia.

Hayati Dkt. Magufuli alifariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena, jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa.

#AzamTVUpdates
Mhariri | @claud_jm

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *