Hotel Verde inayomilikiwa na kampuni za Said Salim Bakhresa (SSB) imeingia miongoni mwa vivutio 20 bora vya utalii duniani (World Travel Award 2025) kutoka Tanzania vinavyowania Tuzo za Dunia za Vivutio Bora vya Utalii.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru amewahimiza Watanzania kuvipigia kura vivutio hivyo ili viweze kushinda tuzo hizo na kusaidia kupanua wigo wa uingiaji wa watalii nchini.
Mhariri @moseskwindi