Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Jijini Mwanza kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambae pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu wa chama hicho na Mwenyekiti wa Kanda Maalumu ya Ziwa Victoria, Ezekia Wenje, leo October 13, 2025 amehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), akitokea Chama Cha CHADEMA.

Wenje akizungumza mbele ya Mgombea Urais wa Tanzania kupitia (CCM), amedai kuwa ameridhishwa na utendaji wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kitendo kilichompelekea kukihama Chama Cha CHADEMA na kuhamia CCM.

#AzamTVUpdates
Mhariri | @claud_jm

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *