Wizara ya mifugo na uvuvi imesema kuwa kwa kushirikiana na Mashirika mbalimbali inatekeleza miradi ambayo inasaidia kukuza Sekta ya uvuvi ikiwepo utoaji wa boti kwa wavuvi ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na pato la Taifa kwa ujumla.
Katika kusherehekea wiki ya Maadhimisho ya chakula duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Jijini Tanga, Wizara ya mifugo na uvuvi kwa kushirikiana na Shirika la chakula Duniani FAO wameandaa mashindano ya kuendesha galawa kwa wavuvi katika Jiji la Tanga ili kutambua mchango wao hasa katika Sekta ya uvuvi
#StarTvUpdates