Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Ziwa, Ezekial Wenje amekihaama rasmi chama hicho na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wanje ambaye pia amewahi kuwa mbunge wa Nyamagana, amekihama chama hicho na kutimkia CCM akisema ameamua kuunga mkono juhudi za maendeleo.
Wenje ametanga uamuzi wa kuhamia CCM leo Jumatatu, Oktoba 13, 2025 akiwa Wilaya ya Chato mkoani Geita mbele ya mgombea urais kupitia CCM, Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye alifika wilayani humo kwa lengo la kuomba ridhaa ya kuchaguliwa tena kuwa Rais.
“natambua duniani kote hakuna nchi ambayo imepata ukomo wa maendeleo,leo nimekuja hapa tpka Mwanza mimi nimesoma Geita Sekondari kipindi nasoma ilikuwa nakuja na basi natumia saa 10 kufika leo nimetumia saa mbili pekee,” amesisitiza Wanje katika mkutano huo
#StarTvupdate