Mgombea ubunge Kwa tiketi ya Chama Cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Agnesta Lambert Kaiza amesema wakazi wa jimbo hilo wanahitaji mabadiliko.
Kwa mujibu wa Agnesta, amegombea katika jimbo hilo ili kuhakilisha analete mabadiliko ambayo wakazi wake wameyakosa kwa muda mrefu kutokana na mbunge aliyekuwapo kuwarudisha nyuma katika maendeleo.
Agnesta amewataka wapigakura hao kumchagua Rais Samia Suluhu Hassan lakini kwa upande wa mbunge na madiwani wakichague Chaumma.
Mgombea huyo amesema hayo leo Jumatatu Oktoba 13,2025 akizungumza katika kipindi cha Bonanza kinachorushwa na Radio Free Africa.
#StarTvUpdate