Katika radiamali kwa makubaliano ya kuhitimisha vita huko Gaza, watumiaji wa mtandao wa kijamii wa “X” wamesema utawala wa Kizayuni umeshindwa kufikia malengo yake dhidi ya muqawama wa Kiislamu wa Palestina, “Hamas.”

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilitoa taarifa siku ya Alkhamisi na kutangaza rasmi kufikiwa kwa makubaliano ya kumaliza vita huko Gaza na kubadilishana mateka. Hamas ilisema: Baada ya mazungumzo mazito yaliyofanywa na harakati na makundi ya muqawama wa Palestina kuhusiana na pendekezo la Rais wa Marekani huko Sharm el-Sheikh lenye lengo la kuhitimisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina na kujitoa kwa wavamizi hao kutoka Ukanda wa Gaza, Hamas inatangaza kufikiwa kwa makubaliano ambayo ni pamoja na kumalizika kwa vita dhidi ya Gaza, kuondoka wazamizi katika Ukanda wa Gaza, kuingia misaada ya kibinadamu na kubadilishana mateka.

Kwa mujibu wa Pars Today, watumiaji wa mtandao wa kijamii wa X kuhusiana na suala hilo wamesema utawala wa Israel kuwa haujafanikiwa kufikia malengo yake dhidi ya Hamas.

Mtumiaji wa mtandao wa X aitwaye “Sadat Husseini” aliandika: “Andika katika historia; kila mtu alikuwa akingojea kushindwa kwa Hamas na kujisalimisha kwa Israel, lakini mwishowe, Israel ililazimika kusitisha mapigano mbele ya muqawama wa Hamas na watu wa Palestina.” “Priya” pia anaamini: “Usitishaji huu wa mapigano utakuwa mgumu kwa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo kwa muda mrefu. Netanyahu aliibebesgha vita Israel lakini hatimaye alijisalimisha kwenye mazungumzo. Israel sio tu haikuangamiza Hamas, lakini wavamizi wake lazima pia waondoke Gaza.

Tutaona katika siku zijazo ni shinikizo gani litakuwa kwa Netanyahu.” “Parvaz,” mwanaharakati mwingine wa X, alibainisha: “Tusisahau kwamba Israel licha ya Israel kutumia teknolojia ya hali ya juu zaidi lakini imelazimika kukubali usitishaji vita dhidi ya Hamas.”

“Yousef” pia alisema: “Mrengo wa mapambano ulishinda na Israel, mtena jinai dunia, imefedheheshwa. Waungaji mkono wa utawala huo wa Magharibi na Marekani walilazimika kusitisha mapigano. Washindi ni watu wa muqawama wa Gaza, Palestina, Lebanon, Iran na Yemen. Israel inaporomoka kutoka ndani.”

Mtumiaji mmoja aitwaye “Ibtihal” pia aliwahutubia Wazayuni na kusema: “Enyi Wazayuni, watu wa Gaza wako pamoja na Hamas na wanaunga mkono harakati hii. Lau si hivyo, watu wangesaliti Hamas tangu siku ya kwanza na kuwakabidhi wanachama wa Hamas kwa Israel.” “Ahmed” aliandika: “Hamas ilisababisha propaganda za Wazayuni kusambaratika duniani kote. Hamas ilifanya kuwaunga mkono watu wa Palestina kuwa kaulimbiu ya wazi katika mitaa ya Marekani na Ulaya. Sasa Israel ndiyo neno linalochukiwa zaidi duniani.”

“Mohammed Talha” pia alibainisha: “Israel ilimwaga damu ya maelfu ya Wapalestina ardhini, na kama si Hamas, utawala huu ungefuta jina na alama ya Palestina.” Na mwisho, Aldo Chaya aliipongeza Hamas akisema: “Wapalestina wa Gaza walisimama imara na thabiti na kukwamisha malengo yote ya Israel, ikiwa ni pamoja na kurejea kwa matela, kuangamizwa kwa Hamas, na kuwatimua Wapalestina kutoka Gaza. Mkakati wa Israel ulifeli na kushindwa vibaya mno”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *