Taasisi za kidini na kielimu, kwa kushirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran, zimefanya mdahalo maalumu jijini Dar es Salaam ukilenga kudumisha amani, mshikamano na haki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.
Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Evangelical Fellowship Church Tanzania, Askofu Charles Asher, amesisitiza umuhimu wa Watanzania kutumia haki zao za kikatiba kwa amani, akisema uchaguzi siyo uwanja wa uhasama bali fursa ya kuimarisha demokrasia.
Ametaka viongozi wa dini kuendelea kuelimisha jamii kulinda umoja wa kitaifa.
Naye Sheikh Mulasar Lulat amewataka Watanzania kujiepusha na uchochezi mitandaoni na kuendeleza misingi ya amani na mshikamano wa taifa.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates