
Kufikia Jumatatu, Septemba 1, Jamhuri ya Shirikisho ya Somalia ina jimbo jipya, Jimbo la Kaskazini-Mashariki, lililoundwa kutoka kwa maeneo yaliyojitenga ya Somaliland ambayo yalipendelea kujiunga na serikali ya Mogadishu. Somaliland ilijitenga na Somalia mwaka 1991 na kujitangaza kuwa jamhuri huru. Tangu wakati huo, haijawahi kutambuliwa kimataifa. Kujitenga kwa sehemu ya eneo lake ni pigo kubwa kwa serikali ya Hargeisa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Gaëlle Laleix
Jimbo la Kaskazini Mashariki linaundwa na mikoa mitatu ya Somaliland: Sool, Sanaag, na Cayn. Tangu mwaka 2023, mzozo wa kivita umekuwa ukiedelea kati ya Mogadishu na serikali ya Hargeisa. Kufuatia kuanzishwa kwa utawala wa mpito, mikoa hiyo mitatu ilimchagua rais wa jimbo lao jipya la shirikisho mwishoni mwa juma hili lililopita.
“Tuko karibu na umoja wa Wasomali leo,” mjumbe maalum wa Somalia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ameshangilia kwenye mitandao ya kijamii.
Mamlaka ya Somalia imewekeza pakubwa katika kuunda jimbo hili jipya. Katika taarifa yake, Waziri wa Mambo ya Ndani ameeleza kuwa alikaa chini kwa mwezi mmoja na nusu ili “kusimamia binafsi” mchakato huo. Mwezi Aprili, Waziri Mkuu alitembelea Las Anood, mji mkuu wa Mkoa wa Sool. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa afisa wa Somalia kutembelea Somaliland tangu mwaka 1991.
Kwa sasa, Somaliland inakaa kimya. “Mazungumzo yanaendelea,” anaeleza Hamse Ibrahim, mtafiti katika Chama cha Baraza la Somaliland. “Hargeisa ina wasiwasi sana; kujitenga huku kunatilia shaka uwezo wake wa kushikilia eneo lake na kufuata sera ya umoja. Ni ishara mbaya kwa uwezekano wa kutambuliwa.”