Kulingana na shirika la uokoaji vifo hivyo vimetokea katika maeneo matatu tofauti ya mgodi huo wa Cuatro Esquinas de Caratal ulioko karibu kilomita 850 kusini mashariki mwa Mji Mkuu Caracas.

Kulingana na idara ya zima moto ya El Callao, operesheni za kuitafuta miili ya watu hao 14 waliofariki zimeanza na idadi hiyo ya imetokana na ushuhuda wa wachimba migodi wengine.

El Callao ni mji unaotegemea uchimbaji wa dhahabu na idadi kubwa ya wakaazi wake 30,000 wanashiriki uchimbaji migodi moja kwa moja au kwa njia zisizo moja kwa moja.

Venezuela ni nchi iliyo na utajiri wa shaba, almasi na madini mengine ila uchimbaji usio salama ni jambo la kawaida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *