
Katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, Biden amesema kwa kuungw amkono na Marekani na washirika wake duniani, Mashariki ya Kati kwa sasa iko katika mkondo wa kupatikana kwa amani.
Biden vile vile amezungumzia dhima ya utawala wake katikamazungumzo ya amani akisema walijitahidi kuhakikisha wanamgambo wa Hamas wamewaachia mateka, kufikisha misaada kwa Wapalestina na kuvisitisha vita hivyo vilivyoanza wakati wa utawala wake mwaka 2023.
Clinton kwa upande wake amesema Trump,Qatar na wahusika wengine wa kikanda waliopelekea kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha vita wanastahili pongezi kubwa.
Ametaka Israel na wanamgambo wa Hamas wadumishe amani ya kudumu.
Clinton amekuwa mkosoaji mkubwa wa Trump akidai sera zake zinatokana na nia za kibinafsi na wala si maslahi ya raia wa Marekani.