Tchiroma amedai kushinda ingawa matokeo rasmi yatatolewa baada ya wiki mbili.

Katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, Tchiroma amesema kuwa ushindi wao ni wa wazi na unastahili kuheshimiwa.

Ameitaka serikali kukubali matokeo au iitumbukize nchi hiyo kwenye machafuko. Tchiroma vilevile ameahidi kuchapisha matokeo ya kina kwa kila eneo.

Biya alikabiliana na wapinzani 11 akiwemo Tchiroma aliyejiuzulu kutoka serikalini mnamo mwezi Juni kujiunga na upinzani baada ya kuhudumu chini ya Biya kwa miaka 20.

Mwaka 2018, mwanasiasa wa upinzani Maurice Kamto ambaye mwaka huu alizuiwa marufuku ya kushiriki uchaguzi na Baraza la Katiba nchini humo, alijitangaza mshindi baada ya uchaguzi.

Alikamatwa baadae na maandamano ya wafuasi wake kutawanywa kwa mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha.

Biya ambaye ndiye kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi duniani, anawania muhula wa nane kama rais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *