Takriban Wapalestina wawili wamejeruhiwa wakati wanajeshi wa Israel walipovamia na kuwafyatulia risasi wakazi wa eneo la Ukingo wa Magharibi. Wanajeshi wa Israel usiku wa kuamkia leo walivamia pakubwa vijii na miji kadhaa ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan

Shirika rasmi a habari la Palestina (WAFA) imeripoti kuwa, wanajeshi wa Israel walimfyatulia risasi mkonononi kijana wa Kipalestina katika mji wa Anabta umbali wa kilomita 9 mashariki mwa Tulkarem na kuwatia nguvuni vijana wengine kadhaa wa Kipalestina baada ya kuwavamia.

Katika tukio jingine lililoripotiwa katika kitongoji cha al -Issawiya huko Quds Mashariki inayokaliwa kwa mabavu na Israel; wanajeshi wa utawala wa Kizayuni walimjeruhi kijana mwingine wa Kipalestina kabla ya kumtia nguvuni. 

Wanajeshi vamizi wa Israel pia walishambulia vitongoji vingine kadhaa katika miji ya Ramallah na al-Bireh mapema leo Jumanne na kuvunja nyumba kadhaa za Wapalestina. 

Vyanzo vya usalama vimearifu kuwaaskari jeshi vamzi wa Israel walivamia nyumba ya Issam al-Froukh huko Ramallah, Mpalestina aliyeachiliwa huru na kuhamishiwa Gaza na kisha kupora vitu na mali za raia huyo. 

Wanajeshi wa Israel waliendeleza hujuma zao hizo na kushambulia vijiji vingine zaidi ya saba walipovamia kijiji cha Deir Ibzi magharibi mwa Ramallah na kisha kuwasaili wamiliki wa vijiji hivyo. 

Zaidi ya Waisraeli 700,000 wanaishi katika zaidi ya vitongoji 230 vilivyoanzishwa tangu utawala wa Israel ilipovamia na kuyakalia kwa mabavu maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds Mashariki.mwaka 1967. 

Jamii ya kimataifa inavihesabu vitongo hivyo vya Wazayuni kuwa kinyume cha sheria kwa mujibu wa sheria za kimataifa na maazimio ya Geneva kwa sababu ya kujengwa kwake katika maeneo yaliyovamiwa na kughusubiwa. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *