
“Viwango vya uharibifu sasa vimefikia karibu asilimia 84, na katika baadhi ya sehemu za Jiji la Gaza, ni hadi asilimia 92,” amesema Jaco Cilliers, Mwakilishi Maalum wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP kwa ajili ya programu za msaada kwa Wapalestina.
Ameongeza kuwa “Tayari tumeondoa tani 81,000 za mabaki sawa na lori zaidi ya 3,100 ili kuruhusu wahudumu wa kibinadamu kufikia watu walio na mahitaji.”
Cilliers amebainisha kuwa wafadhili kutoka ulimwengu wa Kiarabu, Ulaya, na Marekani wameahidi kusaidia juhudi za awali za ujenzi mpya. “Tunaona ishara nzuri kutoka kwa wafadhili, na hii inatoa matumaini kwa miezi ijayo,” ameongeza.
Upatikanaji wa msaada bado ni changamoto
Licha ya msisimko wa kimataifa, utoaji wa msaada umeshindikana kwenye maeneo yaliyoathirika na vita kwa miaka miwili.
Ricardo Pires, msemaji wa Shirika la Umoja wa Maaifa la Kuhudumia watoto UNICEF, amesema “Tunatumai usitishwaji wa mapigano haya ya mwisho utadumu na kuleta amani ya kudumu kwa eneo na kwa Wapalestina. Lakini msisimko kutoka kwa jumuiya ya kimataifa hauonekani kila siku kwenye ardhi hiyo. Hatupati msaada wa kutosha mahali pa muhimu zaidi.”
Mateka na utoaji msaada
Hali hiyo imechangia changamoto za mateka na wafungwa wanaoendelea kwa mujibu wa Jens Laerke msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kutratibu misaada ya Kibinadamu a MMasuala ya Dharura OCHA.
“Jambo la kwanza la kuweka bayana ni kuhusu msaada kufika kwa watu, si watu kwenda kwa msaada”.
Wahudumu wa kibinadamu,likiwemo shirikisho la chama cham salaba mwekundu na mwezi mwekundu ICRC, wamekumbana na changamoto kubwa katika kusambaza msaada kwa usalama ndani ya Gaza.
Mara nyingi, watu wanaporudi kutoka kwenye maeneo ya usambazaji wamejeruhiwa au kifo kimejitokeza.”
Viongozi wa dunia watakiwa kuchukua hatua
Christian Cardon, msemaji wa ICRC, amesisitiza juhudi za kidiplomasia akisema
“Tulikuwepo Sharm el-Sheikh jana na viongozi 22 wa nchi na serikali, tukiwa tunawaomba wasaidie kusukuma kila njia ili kuhakikisha operesheni za msaada zinaanza haraka iwezekanavyo. Tunaendeleza kuhamasisha katika kila ngazi kuhakikisha hili linafanikiwa.”
Umoja wa Mataifaumemetoa wito wa hatua za pamoja za kimataifa kuongeza kasi ya utoaji msaada wa kibinadamu na kuanza ujenzi mpya mkubwa ambao Gaza inahitaji haraka.