
Haya yamesemwa katika taarifa na wizara ya mambo ya kigeni ya mpatanishi wa pande hizo mbili, Qatar.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Qatar, Marekani na Umoja wa Afrikawatashiriki katika mpango huo kama waangalizi tu.
Doha imesema kuwa mpango huo utasimamia utekelezwaji wa usitishwajiwa kudumu wa mapigano, utachunguza na kuthibitisha ripoti za ukiukwaji na kufanya mawasiliano na pande husika kwa ajili ya kuzuia kurudiwa kwa uhasama.
Makubaliano haya ya leo yanafuatia makubaliano ya usitishwaji mapigano ya awali yaliyotiwa saini na pande zote mbili huko huko Doha mnamo mwezi Julai.
Wanamgambo wa M23 walikuwa wanasisitiza kutafuta makubaliano yao wenyewe ya amani na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wakidai makubaliano ya DRC na Rwanda yaliyotiwa saini Juni yaliacha masuala ambayo bado yanastahili kuangaziwa.