
Jeshi la Israel limetangaza jioni ya Jumanne, Oktoba 14, kwamba mateka wengine wanne ambao walikuwa bado wanazuiliwa na kundi la Palestina la Hamas huko Gaza wamekabidhiwa kwa Shirika la Msalaba Mwekundu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika la Msalaba Mwekundu, majeneza manne yenye mabaki ya mateka waliofariki yamesafirishwa chini ya ulinzi mkali na yanaelekea kwa jeshi la Israel na Shin Bet [Usalama wa Ndani wa Israel] katika Ukanda wa Gaza,” jeshi limesema katika taarifa yake.
Baada ya kupokelewa na jeshi, “majeneza (yaliyoingia hivi majuzi) nchini Israel na yanaelekea katika Taasisi ya Kitaifa ya Tiba ,Institut national de médecine légale, (kwa) taratibu za utambuzi,” imesema taarifa ya kijeshi iliyotolewa muda mfupi baada ya saa sita usiku Jumatano (saa 5 uiku Jumanne saa za Ufaransa).