
Pedro Sanchez Waziri Mkuu wa Uhispania amesisitiza kuwa makubaliano ya kusitisha vita Gaza yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na Israel yasifanywe kuwa fidia ya mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Israel Ukanda wa Gaza.
Waziri Mkuu wa Uhispania amebainisha haya katika mahojiano jana Jumanne.
Amesema kuwa: Pande zote kuu husika katika mauaji ya kimbari yaliyofanywa Gaza wanapasa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria ; kinga ya kutoadhibiwa watu hao haipaswi kutolewa.
Mwezi Novemba mwaka jana Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ilitoa waranti wa kutiwa mbaroni Netanyahu na Yoav Gallant Waziri wa zamani wa Vita wa Israel kwa kutekeleza jinai za kivita dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Waziri Mkuu wa Uhispania pia alisisitiza kuwa marufuku ya usafirishaji silaha kutoka na kuelekeka Israel iliyowekwa na nchi hiyo ingali inaendelea. Amesema, Uhispania itaendeleza marufuku hiyo hadi kuimarishwa mchakato wa kupatikana amani.
Uhispania ambayo ni miongoni mwa nchi wakosoaji wakubwa wa mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza Septemba mwaka huu ilitangaza kuwa mwendesha mashtaka wa nchi hiyo kwa kushirikiana na mahakama ya ICC atachunguza “ukiukwaji mkubwa” wa haki za binadamu uliofanywa katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwa uratibu na ICC.
Pedro Sanchez hivi karibuni alitangaza hatua kadhaanchi yake imechkau hatua kadhaa ilu kuzuia mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza.
Hatua hizo ni pamoja na kutoruhusiwa kutumia anga ya Uhispania ndege zinazosafirisha vifaa vya kijeshi kuelekea Israel.