Hamas imerejesha miili ya mateka wengine wanne waliofariki, Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limesema

Hamas imerejesha miili ya mateka wengine wanne waliofariki, Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limesema.

Shirika la Msalaba Mwekundu lilichukua mabaki hayo kwenye majeneza na kuyakabidhi kwa wanajeshi wa Israel usiku wa Jumanne.

Kurejesha huko kumekuja baada ya Israel kuonya kuwa itazuia misaada kauingia Gaza hadi Hamas itakaporudisha miili ya mateka wote 28 waliofariki. Kundi hilo la wapiganaji la Palestina limewarudisha mateka 20 waliokuwa hai na wanne waliokuwa wamekufa siku ya Jumatatu.

Miili ya Wapalestina 45 waliokuwa wanazuiliwa nchini Israel imerejeshwa Gaza siku ya Jumanne, Shirika la Msalaba Mwekundu lilisema katika taarifa yake.

Kwa mujibu wa mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kusitisha mapigano, ambao Israel na Hamas waliukubali, unaitaka Hmas kuwakabidhi mateka wote 48 ifikapo siku ya Jumatatu.

Wakati mateka wote walio hai wakirejeshwa, shinikizo linaongezeka kwa Hamas na serikali ya Israel juu ya mabaki ya mateka 20 ambao Hamas bado hawajawarejesha makwao.

Wapalestina wanazidi kuwa na wasiwasi kwamba kucheleweshwa kwa Hamas kurejesha miili hiyo kunaweza kuleta sintofahamu katika mustakabali wa usitishaji mapigano.
#chanzobbcswahili
#starTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *