Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga amefariki dunia leo asubuhi huko Koothattukulam, wilayani Ernakulam nchini India, baada ya kupata mshtuko wa moyo wakati anafanya matembezi yake ya kila asubuhi.

Hayo yameelezwa na polisi na viongozi wa hospitali alikopelekwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Msemaji wa hospitali ya macho ya Sreedhareeyam Ayurvedic amesema, Odinga, mwenye umri wa miaka 80, alianguka wakati wa matembezi ya asubuhi ndani ya uwanja wa kituo cha tiba cha Ayurveda, na akakimbizwa hospitalini hapo kwenye Kituo cha Utafiti huko Koothattukulam, ambapo alitangazwa kuwa amefariki dunia.

Odinga alikuwa amewasili Koothattukulam siku sita zilizopita, akiambatana na binti yake na wanafamilia wa karibu. Alikuwa akifuata mpangilio wa matembezi ya asubuhi na vikao vya matibabu hospitalini.

Taarifa ya polisi imeeleza kuwa, mwili wake umehifadhiwa kwa sasa katika Hospitali ya Deva Matha.

Kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe nchini Kenya kimejiri siku chache baada ya kaka yake, Dkt Oburu Oginga, kuthibitisha kuwa ndugu yake huyo alikuwa mgonjwa kwa muda, lakini alikuwa akiendelea kupata nafuu akiwa matibabuni nchini India…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *