Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema kanda ya ziwa Ezekiel Wenje ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Nyamagana amesema Chama cha mapinduzi kinamipango ya kweli ya kuwaletea maendeleo Watanzania.
Wenje ametoa kauli hiyo leo Jumatano Octoba 15/2025 katika mkutano wa kampeni za Mgombea Urais wa CCM Dkt Samia Suluhu Hassan Mkoani Kagera alipofika kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Rais kwa kipindi kingine .
Amesema vyama vya upinzani viliruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara na badala ya kunadi sera wakawa wanatoa matusi na kejeli
Aidha amesema baada ya kuona mapokezi makubwa ya wananchi kwa Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na sera zilizo kwenye Ilani ya CCM ya miaka mitano ijayo inaonesha nia ya dhati ya chama hicho kuwaletea maendeleo watanzania.
#StarTvUpdate