Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira amesema kwa mujibu wa takwimu, Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi pekee ambaye amekutana mara nyingi na kuzungumza na viongozi wa vyama vya upinzani nchini. Amesema hatua hiyo inaonesha dhamira yake ya dhati ya kuimarisha maelewano ya kisiasa.

Ameongeza kuwa mazungumzo hayo yamekuwa chachu ya kujenga amani, mshikamano na utulivu wa taifa, mambo ambayo ni nguzo muhimu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Wasira amesisitiza kuwa Rais Samia ameonesha mfano wa kuigwa katika kukuza siasa za maridhiano na umoja wa kitaifa.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *