UCHAMBUZI KUHUSU YANGA: Mchambuzi wa soka @sharif_bayona anasema njia ambazo Yanga SC inapita ni sawa na zile ambazo klabu kubwa duniani inafanya.
Bayona ameifananisha Yanga na Barcelona, akitolea mfano namna Joan Laporta alivyoichukua timu hiyo ikiwa vibaya katika soka na baadae kuiinua.
Mchambuzi huyo anasema mapito ya Rais wa Yanga SC, Hersi Said ni kama vile Laporta wa Barcelona alivyofanya miaka ya 2003.
Bayona anauliza, kama Hersi atakaa Yanga miaka 10, klabu hiyo itakuwa katika ubora gani?
(Imeandikwa na @allymufti_tz)
#Viwanjani