Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limewataka wakazi wa mkoa huo kutoa taarifa za wale wanaotoa vitisho vya kiusalama na…Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limewataka wakazi wa mkoa huo kutoa taarifa za wale wanaotoa vitisho vya kiusalama na…

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limewataka wakazi wa mkoa huo kutoa taarifa za wale wanaotoa vitisho vya kiusalama na kujipanga kufanya vurugu siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 29 mwaka huu ili washughulikiwe kwa mujibu wa Sheria.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Muliro Jumanne Muliro, ametoa wito huo wakati akitoa taarifa ya hali ya kiusalama mkoani humo.

Amesema Oktoba 29 ipo kwa mujibu wa sheria hivyo kila mwananchi ana haki ya kupiga kura na kumchagua kiongozi anayemtaka bila ya hofu na kwamba matishio ya kiusalama hayakubaliki na watakaobainika watashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria.

Katika hatua nyingine Kamanda Muliro amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawashikilia watu wanne kwa tuhuma ya kuendesha Televisheni mtandao bila ya leseni kutoka mamlaka husika.

Amesema waliokamatwa ni Japhet Alex Thobias Mkazi wa Sabasaba Ukonga,wa pili ni Joseph Agustino Mabwe Mkazi wa Sabasaba Ukonga wanaodaiwa kumiliki Wispot Tv. Wengine Tegemeo Zacharia Mwenegoha,Mkazi wa Tabata Ilala mmiliki wa T. Media Two na Elia Costantino Pius Mkazi wa Mbezi Juu Kinondoni mmiliki wa Costa Tv.

Kuhusu mikutano ya kisiasa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema inaendelea vizuri huku hali ya kiusalama ikiendelea kuimarishwa ambapo limewatoa hofu wakazi wa mkoa huo kuendelea na shughuli zao bila ya kuhofia chochote.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *