MASHABIKI WAISIFU AZAMTV KUHUSU PACOME: “Katika hili lazima uwapongeze AzamTV kwakuwa wao ndio wanaoonesha mechi LIVE”
Mmoja wa mashabiki wa Yanga SC, Mbaraka Thabiti amesema kitendo cha mchezaji wa Yanga SC, Pacome Zouzoua kuwa sehemu ya wachezaji walioiwezesha Ivory Coast Kufuzu Kombe la Dunia 2026, AzamTV inapaswa kupongezwa kwakuwa kocha wa taifa hilo ameweza kumuona kupitia mechi zinazorushwa na chombo hicho cha habari.
Pacome alikuwa sehemu ya wachezaji waliocheza jana kwenye mchezo dhidi ya Kenya na Ivory Coast kushinda magoli 3-0.
(Imeandikwa na @allymufti_tz)
#Yanga #Pacome