Hamis Tabasamu, mgombea ubunge wa Jimbo la Sengerema kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi, ameahidi kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijamii katika Kata ya Kagunga ikiwa atachaguliwa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Tabasamu amesema hayo akiwa kwenye mkutano wa kampeni katika Kata ya Kagunga jimbo la Sengerema mkoani Mwanza, Katika Kata ya Kagunga ,amesema kuwa atahakikisha kila kitongoji kinanufaika na Maendeleo hususani miundombinu bora, huduma za afya, elimu bora, umeme na maji safi na salama.
Tabasamu amemaliza kampeni zake katika Kata 26 na sasa anaendelea na mikutano katika mitaa na vijiji, akijitahidi kutoa sera zake za maendeleo kwa wananchi.
Pia, mgombea huyo wa ubunge ameendelea kumuombea kura kwa wananchi wa jimbo hilo mgombea urais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza kuwa uchaguzi huu ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
#StarTvUpdate