Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Bara, Ndg. Mussa Peter Mwakitinya, amesema nia ya mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kukuza uchumi na kuboresha ustawi wa Watanzania.

Akizungumza Wilayani Nyang’hwale, Mkoani Geita katika muendelezo wa kampeni za kumuombea kura Dkt. Samia, Mwakitinya amesema CCM inalenga kuongeza ajira kwa vijana, kuongeza kipato kwa wananchi na kuondoa umasikini.

Amesema chama hicho kitaendelea kuboresha huduma za afya, umeme na maji, akisisitiza kuwa Dkt. Samia anaongoza kwa dira ya maendeleo na ustawi wa kila Mtanzania.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *