NAIROBI – Mwili wa Waziri Mkuu wa zamani nchini Kenya, Raila Odinga, umewasili jijini Nairobi muda mfupi baada ya saa 10Am asubuhi kwa majira ya Afrika Mashariki, siku moja baada ya kufariki dunia akiwa Kerala, nchini India.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa Odinga na viongozi wa tabaka mbalimbali wakiongozwa na rais wa Kenya, William Ruto, rais mstaafu Uhuru Kenyatta, na naibu rais Kithure Kindiki, wameupokea mwili wa Odinga. Shughuli katika Uwanja wa Kimataifa wa JKIA zilisitishwa kutokana na idadi kubwa ya wafuasi wa Odinga waliojitokeza kupokea mwili wake. Mamlaka za viwanja vya ndege nchini Kenya zilitangaza kusitisha shughuli za kawaida ikiwemo kupaa na kutua kwa ndege kwa muda.

Wafuasi wa Raila jijini Nairobi, 16 10 2025
Wafuasi wa Raila jijini Nairobi, 16 10 2025 REUTERS – James Keyi

Kifo cha Raila kimesababisha raia wengi kujitokeza mitaani kuandamana, kama njia ya kumuenzi, huku maswali yakiibuka kuhusu jinsi siasa za Kenya zitakavyokuwa bila Odinga kuwepo.

Misa ya kitaifa ya kumuombea Raila itafanyika kesho katika uwanja wa Kitaifa wa Nyayo, jijini Nairobi, ambapo viongozi wa tabaka mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria. Tayari serikali ya Kenya imetangaza kesho kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa.

Mfuasi wa Raila akilia
Mfuasi wa Raila akilia REUTERS – Monicah Mwangi

Siku ya Jumamosi, mwili wa Raila utasafirishwa na kupelekwa katika jiji la Kisumu, lililokuwa ngome yake kisiasa, kabla ya ibada ya mazishi itakayofanyika siku ya Jumapili. Kwa mujibu wa kamati ya kitaifa inayoshughulikia mazishi ya Raila chini ya naibu rais Prof. Kithure Kindiki, Raila aliacha wasia akitaka azikwe siku tatu baada ya kifo chake, kando ya kaburi la mamake mzazi Mary Juma Odinga, katika shamba lake la Opoda, Bondo, Kaunti ya Siaya.

Wafuasi wa Raila jijini Kisumu
Wafuasi wa Raila jijini Kisumu REUTERS – Thomas Mukoya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *