Wagombea wa nafasi ya Ubunge Eng. Chacha Wambura na Udiwani Kata ya Nyanguku Elias Ngole katika jimbo la Geita Mjini wamesema wakipata nafasi ya kuwaongoza Wananchi watahakikisha suala la barabara linatatuliwa kwa zile ambazo zotaboreshwa na zile zinazohotajika kuwekwa lami.
Mgombea udiwani wa kata hiyo Elias Ngole ameeleza kuwa moja ya vipaumbele vyake vikuu ni kuhakikisha barabara za ndani ya kata ya Nyanguku zinafunguliwa na kuboreshwa, ili kurahisisha usafiri na upatikanaji wa huduma muhimu kama elimu, afya, na masoko.
Mgombea Ubunge Jimbo la Geita Mjini amewahakikishia Wananchi kwa kushirikiana na Madiwani watahakikisha barabara zinapitika hata kama itamlazimu kukodi vifaa vya kufanya hivyo.
Aidha, amewaomba wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi katika mikutano ya kampeni na hatimaye kuchagua viongozi wanaowajali, watakaosimamia miradi ya maendeleo kwa vitendo na si maneno.
#StarTvUpdate