Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtama, Nape Moses Nnauye amewataka wananchi wa mji wa Shuka, uliopo jimboni humo kutouza ardhi yao ovyo, akisisitiza kuwa eneo hilo lina thamani kubwa kutokana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.
Akizungumza na wakazi wa Shuka, katika kampeni zake za kitongoji kwa kitongoji, Nape amewahakikishia wavuvi na wadau wa sekta hiyo kuwa serikali imejipanga kuboresha mazingira yao ya kazi, ikiwemo ujenzi wa vizimba vya kuhifadhi samaki na miundombinu mingine ya kisasa.
Aidha, amebainisha kuwa ardhi ya mji wa Shuka inaendelea kupanda thamani kutokana na mpango wa serikali wa kujenga barabara mbadala itakayounganisha mikoa ya Kusini na Pwani kupitia eneo hilo.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates