“Nilimwambia mke wangu anishike shingoni tujitahidi kutoka…lakini ghafla mkondo mkali wa maji ulimchukua…nilijitosa kumtafuta, sikumpata.” 😢 – Hilario Reynosa Valderas akisimulia namna yeye na mkewe Elodia Reyes Azuara walivyonusurika katika mafuriko yaliyolikumba jiji la Poza Rica, nchini Mexico.
Kwa bahati nzuri, alimuona akijitokeza tena juu ya maji. “Asante Mungu, yuko hai,” anasema Hilario kwa sauti ya shukran. 🙏
Picha zilizopigwa na majirani zimewaonesha wanandoa hao wakiwa wamekumbatiana huku wakiwa wamezungukwa na maji yaliyosababisha vifo vya watu kadhaa jijini humo. 💔
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi