Mgombea ubunge wa Arusha Mjini kupitia CCM, Paul Makonda, ametaja vipaumbele vyake, endapo atachaguliwa kuwa mbunge kuwa ni kukuza uchumi, kujenga miundombinu na kuboresha huduma za kijamii.

Akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Krokoni, Makonda amesema atahakikisha Arusha inakuwa kitovu cha maendeleo kwa kuvutia wawekezaji, kujenga viwanda na hospitali ya kitalii, sambamba na kuboresha barabara, shule na vituo vya afya ili kuinua maisha ya wananchi.

✍ Mwandishi Wetu
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *