Katika maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Jijini Tanga, Mamlaka ya udhibiti wa nafaka na mazao mchanganyiko (COPRA) waliandaa mashindano ya mama lishe katika upishi wa vyakula mbalimbali Ikiwa lengo ni kuhamasisha wannachi kutumia vyakula vya asili ili kuimarisha Afya zao.
Vyakula vilivyoshindanishwa ninamna ya kupika choroko, mbaazi, kunde, dengu na washindi waliofanikiwa kupika vyakula hivyo wamepatiwa zawadi ya pesa pamoja na majiko ya gesi.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa nafaka na mazao mchanganyiko COPRA, Irene Mlola amesema mama lishe hao watatumia ujuzi walioupata kupitia Mafunzo walioyopatiwa ili kuhamasisha wananchi kuendelea kutumia mazao ya asili.
Pia Mlola amesema Serikali imajipanga kuhakikisha inakuza soko la vyakula hivyo hapa nchini ili Watanzania waweze kutumia mazao hayo kupata lishe bora.
Maadhimisho hayo yamehitimishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye amezitaka Halmashauri zote Nchini kutenga bajeti katika masuala yote ya lishe hapa nchin.
#StarTvUpdates