Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Profesa Neema Mori amewakaribisha wawekezaji wa kimataifa kuja kuchangamkia fursa za kiuchu...

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Profesa Neema Mori amewakaribisha wawekezaji wa kimataifa kuja kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo nchini na ukanda wa Afrika Mashariki huku akiwahakikishia kuungzwa mkono na Benki ya CRDB.

Profesa Mori ametoa wito huo kando ya Mkutano wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF) unaoendelea jijini Washington nchini Marekani akisisitiza kwamba Benki ya CRDB ni daraja makini kati ya mitaji ya kimataifa na masoko yanayokua kwa kasi barani Afrika kwani tayari inao uzoefu wa kuhudumia Tanzania, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

“Tunaona fursa kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki, na Benki ya CRDB imejipanga kuwa mwezeshaji wa uwekezaji katika madini, utalii, viwanda na kilimo; sekta ambazo ni injini ya ukuaji wa uchumi wa bara letu,” amesema Profesa Mori.

Ameongeza kuwa Uwezo wa kifedha, mtandao wa kikanda walionao benki ya CRDB, pamoja na mifumo madhubuti vinatoa uaminifu unaohitajika na wawekezaji wanapotafuta mshirika wa benki ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *