Ubalozi wa China mjini Washington umesisitiza kuwa, kuwekwa vikwazo vya upande mmoja na mashinikizo mengine yoyote kutoka kwa serikali ya Marekani hakutaathiri ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Russia.

Taarifa ya ubalozi wa China mjini Washington imetolewa kujibu matamshi ya Donald Trump ya kuitaka Beijing iache kununua mafuta ya Russia.

Liu Pengyu, msemaji wa ubalozi wa China mjini Washington ameziambia duru za habari kwamba, “China inakataa kwa nguuvu zote vikwazo vyovyote visivyo halali vya upande mmoja, hatua za kulazimishwa na shinikizo kwa namna yoyote.

Mwanadiplomasia huyo ameongeza kuwa, ushirikiano wa China unafanyika katika fremu ya mfumo wa jamii ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na nchi rafiki – Russia, ni wa kimantiki na wa kisheria unaozingatia sheria za kimataifa, haudhuru maslahi ya upande wa tatu, na unapaswa kuheshimiwa na kuungwa mkono.

Ubalozi wa China pia umetangaza kuwa Beijing iko tayari kwa vita vya kibiashara na Marekani, lakini pia iko tayari kuzungumza. Taarifa hiyo imesisitiza kuwa Marekani haiwezi kudai suluhu ya mizozo kwa upande mmoja na kuweka shinikizo kwa nchi nyingine kwa kutishia kuziwekea ushuru wa forodha.

Marekani inapinga vikali kuimarishwa mfumo wa kambi kadhaa na inajaribu kudumisha nafasi yake ya kupenda vita kimataifa kwa kutumia mabavu na kulazimisha matakwa yake kwa nchi nyingine; na katika mchakato huo inanufaika na msaada wa baadhi ya washirika wake wa Magharibi.

Pamoja na haya yote, ushahidi unaonyesha kutengwa Marekani kwa sababu ya hatua na maamuzi ya upande mmoja na ya mabavu ya Trump na hivyo kupungua kwa nafasi kuu ya Magharibi duniani chini ya uongozi wa Marekani. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *