Rais Masoud Pezeshkian wa Iran ameashiria uwezo wa kustaajabisha wa vijana wa Jamhuri ya Kiislamu na kusisitiza kuwa, vijana wa taifa hili ndio ambao wanetengeneza makombora na nishati ya nyuklia kwa kutegemea uwezo wao.

Rais Pzeshkian aliyasema hayo jana Alkhamisi akiwa ziarani mkoani Isfahan, katikati ya Iran ambapo amesisitiza umuhimu wa kuimarisha hali ya kujitegemea ili kuisaidia nchi hii kufikia malengo yake makubwa.

“Lazima tujenge na kuimarisha imani kwamba ‘tunaweza’,” Pezeshkian alisema katika hafla ya kukuza harakati za ujenzi wa shule katika mkoa huo wa kati.

Pezeshkian amewataka maafisa wa serikali kupiga jeki juhudi zinazoonekana katika maendeleo ya taifa, akisema kwamba mamlaka lazima itengeneze mazingira ambapo uwezo wa watoto wa Iran unaweza kustawi.

Aidha Rais wa Iran amesisitiza kwamba, kwa umoja wa wanancchi, hakuna nguvu kutoka nje inayoweza kulidhoofisha taifa hili la Kiislamu.

Dakta Pezeshkian pia ameashiria uungaji mkono wa wananchi wa Iran kwa Jamhuri ya Kiislamu wakati wa vita vya 12 vya kutwishwa na utawala wa Israel mwezi Juni, akisema kwamba maadui walikuwa na matumaini kwamba Iran imedhoofika, na kwamba wanaweza kulishambulia taifa hili.

Amesema, hata hivyo, maadui hawakujua ukweli kwamba watu wanaposimama kwa umoja, hakuna nguvu inayoweza kuwaangusha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *