Russia. Kama ilivyo kwa watu wazima, watoto hupata maambukizi ya mfumo wa mkojo kitabibu Urinary Track infection (UTI).

Haya ni maambukizi ya bakteria katika sehemu yoyote ya mfumo wa mkojo, ikiwa ni pamoja na figo, kibofu na mirija iliyounganishwa nayo.

Bakteria wajulikanao kitabibu kama E.Coli ndio kisababishi kikuu, huchangia takriban asilimia 80 ya UTI kwa watoto na zaidi kwa watoto wa kike kuliko wa kiume kutokana kuwa na mrija mfupi.

Bakteria hao wa kwenye utumbo mpana huingia kwenye mrija wa mkojo yaani urethra hatimaye katika kibofu.

Habari nzuri za kitakwimu ni kuwa UTI haijakuwa tishio kama ilivyo kwa magonjwa kama malaria, nimonia na kuharisha ambayo ndio yanaongoza kusababisha vifo vingi duniani.

Pili ni usafi duni, itakumbukwa kuwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, hasa miaka mitatu hushindwa kudhibiti haja hivyo kujisaidia.

Vilevile kuchelewa ubadilishaji wa nepi, chupi au diaper pamoja na uoshaji au ufutaji usiozingatia maelekezo ya wataalam wa afya, yaani kufuta kutoka nyuma kwenda mbele kwa watoto wa kike.

Sababu ya tatu ni tabia za kukojoa, kubana na kushikilia mkojo kwa muda mrefu hii inaweza kuruhusu bakteria kukua. Ikumbukwe kuwa kukojoa mara kwa mara husaidia kuwatoa nje.

Nne ni tatizo la kuvimbiwa, ulaji au ulishwaji holela ni kawaida watoto kupata hali hii, hivyo kusababisha kuongezeka kwa haja kubwa kunakoweza kuongeza hatari.

Tano ni watoto kutokunywa maji ya kutosha na kusababisha mkojo kujilimbikizia zaidi katika kibofu na kufanya kuwa vigumu kwa mwili kuwatoa bakteria kwa njia ya kukojoa.

Mambo hatarishi yanayochangia UTI ni pamoja na tofauti za kimaumbile; wa kike wana mrija mfupi na ukaribu na haja kubwa hivyo ni rahisi bakteria kuingia kwenye kibofu.

Vile vile wavulana wasiotahiriwa bakteria wanaweza kujilimbikiza chini ya mkono wa sweta.

Pia kutokana na kuogeshwa na sabuni zinazowasha hatimaye mrija wa mkojo kuvimba hatimaye kuunda makazi njia ya kuingilia kwa bakteria. 

Kwa watoto wachanga na watoto wadogo dalili zisizo maalum ni kama vile homa, kuwashwa, kutapika, kuhara na kutokuwa sawa kwa ujumla.

Watoto wakubwa wanaweza kukojoa mara kwa mara, maumivu,  kuwaka moto wakati wa kukojoa au kutokwa na mkojo wenye mawingu au harufu mbaya.

Ili kupunguza hatari watoto kupata UTI inatakiwa kumfundisha kwa vitendo, ili kumjengea mazoea ya kukojoa mara kwa mara na unywaji wa maji ya kutosha. 

Wazazi, walezi na wasaidizi wa watoto wahakikishe ufutaji sahihi yaani kutoka mbele kurudi nyuma baada ya kutoka haja au baada ya kujisaidia.

Baini viashiria vya mtoto kujisaidia, ili kumsafisha na kumbadilisha nguo ya ndani mapema. Mvalishe nguo za ndani zenye asili ya pamba kwani ni nzuri  zaidi kwa usafi wa mwili.

Mfikishe mapema katika huduma za afya pale unapopata dalili ili kuzuia maambukizi makubwa zaidi ya figo. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *