#HABARI: Mahakama Kuu Kanda ya Tanga imewahukumu Hamisi Jamali Mkufya (22) na Abdallah Sebo (20), wakazi wa Mbugani, kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kulawiti msichana mwenye umri wa miaka 16, mkazi wa Mikanjuni, Wilaya ya Tanga.
Tukio hilo lilitokea Desemba 26, 2023, na baada ya kuripotiwa polisi, watuhumiwa walikamatwa na upelelezi kuanza mara moja. Desemba 27, walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tanga, kabla ya jalada kuhamishiwa Mahakama Kuu chini ya kesi namba CC No. 27880/2024, mbele ya Jaji Kobelo, ambapo walikana mashtaka.
Baada ya ushahidi thabiti kutoka upande wa mashtaka, Mahakama iliwatia hatiani na mnamo Oktoba 16, 2025, ikawahukumu kifungo cha maisha.
Uamuzi huu umetafsiriwa kama hatua ya kuweka mfano kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na kulinda haki za waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania