#HABARI: Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Felista Njau, ameibukia katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika mjini Bunda, ambapo alimnadi mgombea ubunge wa CCM katika jimbo hilo Esther Bulaya, huku akitoa wito kwa wananchi kumpigia kura Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema “zipo sababu milioni moja za kufanya hivyo.”

Katika hotuba yake iliyopokelewa kwa shangwe, Felista amesema kuwa Rais Samia amethibitisha kuwa ni kiongozi wa vitendo na mwanamke mwenye dira, aliyetekeleza kwa ufanisi Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020/2025.

Akizungumzia sekta ya utalii, Felista alimtaja Rais Samia kama balozi wa kisasa wa Tanzania, aliyebadilisha taswira ya taifa kimataifa kupitia filamu ya Royal Tour.

“CCM iliahidi kupata watalii milioni tano. Samia akaingia porini akacheza filamu ya Royal Tour — leo tunajivunia zaidi ya watalii milioni 5.36. Ilani imetekelezwa kwa asilimia 100,” aliongeza.

Mbunge huyo mstaafu pia alitaja hatua za Rais Samia katika kuboresha huduma za afya, hasa kwa akinamama wajawazito na watoto.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *