Dar es Salaam. Gwiji wa muziki wa taarabu nchini, Mzee Yusuf amesema sababu ya kuwajibu mbovu watu kwenye mitandao ya kijamii ni hali ya udhaifu inayomtokea kama mwanadamu kwani wakati mwingine uvumilivu unakuwa unamshinda pale mashambulizi dhidi yake yanapozidi.

Akizungumza na Mwananchi Mzee Yusuf amesema anachukizwa na watu wanaotukana wenzao mitandaoni ndiyo maana uvumilivu wakati mwingine humshinda na kujikuta akimtolea uvivu mtu anayembeza kwa kurudi kwenye kuimba taarabu baada ya awali kutangaza kuacha maisha ya kidunia na kumrudia Mungu.

“Unajua tunawapenda sana mashabiki wetu, lakini kuna wakati wanatukosea, unakuta mtu ametoka alikotoka huko anakukomentia matusi kwenye picha au video uliyoiweka kwenye akaunti yako, tena hicho kitu kilichowekwa unaweza kukuta ni tangazo la kazi yangu, kiukweli sitakubali kutukanwa.

 “Mimi ni mpole lakini sipendi upole wangu unifanye kutukanwa tu, kwani kurudi kwenye kuimba ndio sababu ya wao kunitolea matusi, kama ni kuhukumiwa basi wamuachie muhusika anayetoa hukumu afanye kazi yake na sio wao, nitachukua hatua kwasasa sitawaacha,” amesema Mzee Yusuf.

Mwaka 2016 Mzee Yusuf aliamua kuacha kuimba muziki wa taarabu, akaenda kuhiji na kujikita katika masuala ya dini ya Kiislamu na kuimba Qaswida. Lakini ilipofika mwaka 2020, alirudi kwenye taarab akisema shida zimemrudisha mjini.

Mzee Yusuf amewahi kinara wa muziki wa taarabu nchini akitamba na nyimbo kama, Daktari wa Mapema, Nitadumu Naye, Mpenzi Chocolate, My Valentine, VIP na nyinginezo nyingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *